Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Wednesday 8 May 2013

HOTUBA YA MALKIA WA UINGEREZA IMESISITIZA MABADILIKO KTK SHERIA ZA UHAMIAJI NA MASWALA YA KIUCHUMI
The Queen at the state opening of Parliament


Serikali ya Uingereza imeweka sheria za uhamiaji na maswala ya uchumi kama kipaumbele cha shughuli zake ktk kipindi cha bunge kinachokuja na ambacho kilianza Jumatano kwa hotuba ya Malikia Elizabeth 11.

Hotuba hiyo iliweka wazi nia ya serikali ya kuendelea kurekibisha sheria za uhamiaji  ambapo sheria kali dhidi ya wahamiaji haramu zitatungwa. Alifafanua kwamba sheria hizo zina malengo ya kuhakikisha kwamba wahamiaji wanaifaidisha nchi na sio kufadika wao tu. Pamoja na mambo mengine sheria za uhamiaji zitakusanya vipengele ambavyo vitarahisisha kusafirishwa wote ambao wataonekana kua hawana haki ya kuishi nchini.

Kwa upande mwengine uamuzi huo unapingwa na baadhi ya wanasheria kama vile Yvette Cooper wa chama cha upinzani cha Labour ambae amelaumu sheria hizo kwa madai kwamba,  zimeshindwa kuelezea hali za udhalilishaji wanazofanyiwa wahamiaji haramu na watu wanaofanya kazi kinyume cha sharia. Alitetea hoja yake hiyo kwa kusema 'wahamiaji ni muhimu kwa Uingereza ispokua ipo haja ya kujaribu kudhibiti ili uadilifu utendeke kwa wote'.

No comments:

Post a Comment