Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Friday 29 March 2013

NAIBU SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA NA BAADHI YA WABUNGE WAKUTANA NA WATANZANIA LONDON


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania,  Mh. Job Ndugai.
 

Baadhi ya Wahudhuriaji
 
 
Baadhi ya Wahudhuriaji

WaTanzania wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge.
 
 
Hakimu Mkazi wa Bagamoyo Saidi Mkasiwa  (anaesoma Masters hapa UK) akiuliza swali.
 
Nd. Shabani Kawawa nae alikuwa na machache ya kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge.
 
Baadhi ya WaTanzania
 
Ndugu Abeid Khamis akijieleza
 
kusikiliza kwa makini


kikao cha mbele
 

 
Bi Mariam Mungula (KATIBU CCM-UK na TAWA ) aliendesha Kikao hicho kwa idhini ya Naibu Spika Mh. Ndugai
 
Naibu Spika na Dr Mohammed wakifurahia jambo, kikao kilifana sana.
 
Mama Beatrice Shelukindo , Mbunge wa Kilindi akielezea jambo kwa umahiri .


Mh. Godfrey Zambi , Mbunge  wa Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya
Mh. Salehe Pamba Mbunge wa Pangani na Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini

 
Naibu Spika akifurahia jambo na pembeni yake ni Katibu wa East African Education Foundation Dr. Mohammed Zaharani.
 
Mama Beatrice Shelukindo, Mbunge

Attentive listening ....
 
 
Mwenyekiti wa TAWA Bi Mariam Kilumanga akiwa amekaa pembeni ya Mariam Mwenziwe na Mh. Beatrice Shelukindo.

Meza Kuu au wa mbele  wa kwanzan kulia ni Mh. Salehe Pamba , akifuatiwa na Dr. Mohamed Zaharani , wa Katikati ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania , akifuatiwa na Bi Mariam Mungula (Katibu wa CCM - UK, na Katibu wa TAWA UK ), pembeni  ya Bi Mungula ni Mh. Godfrey  Zambi na wa Mwisho kwenye jopo hili ni Nd. Haruna Mbeyu ("Special Advisror" wa CCM -UK  na Meya wa London)
 
 
Jopo la Mbele , akiwemo Naibu Spika Mh. Job Ndugai -wakimsikiliza maelezo kutoka kwa Mh. Pamba.
 

Kikao kilikuwa kizuri sana  Naibu Spika na Waheshimiwa Wabunge wengine licha ya kuchoka kutokana na ratiba yao ndefu waliyokuwa nayo mchan ule , walifurahi sana na kuwafariji Watanzania kwani walikuwa wazi kujadili mambo mengi kwa kina bila ya kujali kesho yake wanahitaji kuondoka mapema....
 


Mh. Pamba Mbunge wa Pangani na Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
 
 
Hapo sasa Special Advisor CCM UK akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mbeya.

Mheshimiwa Zambi alifunguka kana kwamba anatoa hoja Bungeni .....au ni vile viti na Zulia vyekundu ? safi sana
 

Nyuma kwa mbali mwenye  pink ni Nd. Saidi Yakubu wa Bunge . anaemfuatia ni Nd. Khamis na kwa mbele blogger Jestina George akiwa na Mfanyabiashara Hilal.
 
 
Mr & Mrs "Doctor" nao hawakupitwa .

M/kiti wa TA UK , Saidi Surur na kwa nyuma Mabinti wa Tanzania Amina na Safina .
 


 



 

 
Kikao hiki kisingewezekana bila ya jitihada zako Meya , Asante sana kwa kazi nzuri  kutoka kwa TwigaVoice Team.
 
Mama Beatrice Shelekindo
 
Mwaga sera Meya , mwaga sera.
 
Dr. akielezea .
 
Meya wa London Nd.Haruna Mbeyu akimwaga sera.
 
Vote of Thanks kutoka kwa Meya wa London , Haruna Mbeyu.


Picha ya pamoja
 

Picha ya pamoja Mh. naibu Spika (katikati waliokaa) na Wabunge wote na baadhi ya WaTanzania wakiwakilisha.

 
picha za pamoja

 
Waheshimiwa Wabunge na Nd. Saidi Yakubu
 
WaTanzania wa UK wakiwa na Wabunge.
 
Wakina mama na Mh. Wabunge
 
Mwenyekiti wa Wanawake Bi Mariam Kilumanga akiwa na Mh. Naibu Spika Job Ndugai.
 

Naibu Waziri Spika Mh. Job Ndugai akiongozana na Baadhi ya Wajumbe wa Tume ua Utumishi wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano Tanzania
Waliwapa fursa baadhi ya WaTanzania wanaishi maeneo ya mji wa London kuonana nao na kubadilisha nao machache.
Kikao hichi kilifanyika katika Hoteli ya Park Plaza iliyopo karibu na Majumba ya Bunge la Uingereza , Westminster Houses of Parliament.
Naibu Spika na Tume ya Utumishi walikuwa Uingereza kwa Mualiko wa Naibu Spika wa Uingereza.
WaTanzania hao waliokuwa na shauku ya kuonana na baadhi ya Wabunge Wao, walipata nafasi ya kubadilishana mawazo na Mh. Naibu Spika na baadhi ya Wajumbe aliefuatana nao akiwemo Mh. Beatrice Shelukindo, Mh.Godfrey Zambi na Mh. Salehe Pamba.
Naibu Spika aliwashauri WaTanzania waishio Uingereza kuwa wawe wamoja na kuwa mstari wa mbele katika kuisemea Tanzania vizuri hususan nje na nchi. vilevile WaTanzania waliaswa wawe makini na wachambuzi wa mambo kwani mara nyingi habari zinazoandikwa huwa hazina ukweli ndani yake hivyo kutafuta njia tofauti za kupata habari halafu kufanya tathmini ili kupata ukweli.
 
 Kwa Ujumla WaTanzania waliohudhuria walipata nafasi ya kuuliza  maswali tofauti yanayohusiana na utendaji kazi wa Bunge na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambayo yalijibiwa kwa maelezo ya kina kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge hao na kuweza kukonga nyoyo za WaTanzania waliokuwapo na kuwapa fursa ya kuelewa jinsi ya utendaji kazi wa Wabunge wao. Wa Umoja WaTAnzania hao walifarijika na kukubali kuwa Mkutano huu ingawa ulikuwa ni wa dharura ulikuwa na manufaa sana kwani waliweza kupata maelezo ya kutosha na yenye uhakika kuhusiana na mambo mengi yanayoendela nyumbani Tanzania na walidhamiria kuchukua ujumbe wa siku hii na kuwa  mabalozi wa kuelewesha wenzao pale inapobidi.
 
HABARI NA TWIGAVOICE TEAM.
 
 
 

No comments:

Post a Comment