Habari NA Neema Malley
Baadhi ya watu waliowahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa
...Waokoaji
Juhudi zinaelekea kulala.
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
(PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO, HABARI MSETO BLOG & AUDIFACE BLOG
MIILI ya watu wawili imepatikana na majeruhi 13
pamoja na magari manne kwenye eneo la kisutu mtaa wa
Indira Gandhi na Morogoro road ambapo jengo la
ghorofa 16 limeanguka na kusababisha hali ya
taharuki kwa wakazi wa eneo hilo .
Kwa mjibu wa bango lilikuwepo katika eneo
lilionyesha kuwa jengo hilo linamilikiwa na Shirika
la Nyumba NHC na Ladha Contruction ambalo lilikuwa
linajengwa na Luck Contruction ambapo lilisajiliwa
na Contructor Registration Board(CRB).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa Bw.Meck Sadik alisema tukio hilo saa
2:46 asubuhi ambapo linakadiriwa kuwa na watu zaidi
ya 60.
Bw.sadiki alisema anashindwa kuzungumzia chochote
kwa ufasaha kutokana kuwa bado mapema hivyo
aliwataka waandishi na wananchi kuwa na subira
wakati uokuaji unaendelea.
Mbali na hali hiyo pia kulisikika sauti za watu
kutoka chini ya kifusi wakiomba msaada wa kuokolewa
ndipo mmoja wa askari aliyekuwa ameshika kipaza
sauti aliwatuliza wahanga hao.
"Tulieni watanzania wenzenu wapo hapa kwa ajili ya
kuwaokoa poleni sana kwa uchungu mnaoupata mtatoka
mkiwa hai"alisema askari polisi.
Sambamba na hilo ingawa raia walionekana kuwa na
majonzi lakini walikuwa mstari wa mbele kuwasaidia
waokoaji kuhakikisha waliofunikwa na kifusi
wanaokolewa wakiwa salama.
Kabla ya hapo jeshi la polisi liliwazuia watu
wasishughulike na kitu chochote ila baadaye
wakaonekana kuhelemewa ndipo saa 5:17 wananchi
walilivamia eneo hilo na kuanza kuokoa.
Katika eneo la tukio zoezi la uokoaji lilionekana
kuwa zito kutokana hofu ya kuwafunika walio hai
ambao wamefunikwa na kifusi.
Majira ya Saa 6 Mchana Jeshi la Wananchi(JWTZ)
pamoja na Jeshi la kujenga Taifa(JKT) walionekana
katika eneo la tukio wakipanda juu ya kifusi la
jengo lililoanguka bila vitendea kazi ambapo baada
ya dakika chache walionekana kushuka hali
iliyoashilia ni kutokana na kutojuwa nini la
kufanya.
Hivyo kutokana na ukosefu huo JWTZ pamoja na JKT
mpaka saa 7 mchana walijikuta wanaungana na wananchi
kupanga mstari mmoja ambapo walikuwa wanaokota
tofari moja moja wakiwa wanapasiana.
Mbali na hilo uhaba wa vitendea kazi lilikuwa ni
moja ya tatizo lililokwamisha zoezi hilo kwa kiasi
kikubwa pamoja na hofu ya kuwafukia waliochini
ambapo wapo hai.
Kwa upande mwingine Jeshi la zimamoto lilionekana
likimwaga maji kupunguza fumbi kwa waokoaji pamoja
na walio chini ya kifusi.
Huduma ya maji ilikuwa inatolewa bure ili kupunguza
kiu kwa waliokuwepo katika eneo la tukio pamoja na
hali ya ulinzi iliimarika kwani jeshi la kutuliza
fujo(FFU) walionekana na mbwa wa usalama .
Mpaka mchana viongozi mbalimbali waliudhuria katika
eneo la tukio akiwemo rais Kikwete,Mkuu wa Mkoa,Mkuu
wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam
Kamanda Suleiman Kova .
No comments:
Post a Comment