Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Friday, 29 March 2013

WITO WA KURIPOTI UNYANYASAJI WA KIJINSIA ...

Na Neema Malley

WANAWAKE nchini wametakiwa kuondoa hofu ya kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kuhusiana na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kuliko kusubiri athari kubwa kutokea .

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na mratibu mradi wa utoaji elimu ya jinsia na usimamizi wa kupambana na ukatili wa wanawake majumbani Bw.Suleimani Mtende alipotoa elimu kwa wajumbe wa mabaraza kwa kata ya Mgulani,Keko ,Azimio ,kurasini pamoja na kata ya mtongani.

Aidha Bw.Mtende alisema kuwa dhumuni kubwa la mkutano huo nikutoa elimu kwa wajumbe wa baraza kuhakikisha wanasimamia hatua zinachukuliwa juu watu wanaofanya matukio ya unyanyasasi wa kijinsia.

"Wajumbe waliopo kwenye mkutano huu wawe ndo chachu ya kuweza kutatua tatizo hili katika jamii zetu na kufanikisha swala la unyanyasaji wa kijinsia kutokomea "alisema Bw.Mtende

Pia Mratibu wa jinsia kutoka katika taasisi ya SAREPTA WOMEN GROUP ambao ndo waratibu wa huo mradi Bibi Juliath Haule alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo katika jamii kwa sasa ni wanaume kushindwa kuripoti matukio ya unyanyasaji wanayofanyiwa katika vyombo vya hata kama wapo wamaoripoti niwachache ukilinganisha na wanawake.

"Tumekuwa tukiegemea upande wakina mama peke yake ndio wanakutwa na matukio ya unyanyanyasaji wa kijinsia ambapo jambo hilo si kweli kuna wanaume kibao wanaopata manyanyaso ila hawaendi kuripoti katika vyombo vya sheria" alisema Bibi Haule.

Pia aliongezea kwa kusema kuwa inabidi jamii ichukue hatua kali juu ukatili wa kijinsia kwani unaonekana ndio moja ya sababu za maambukizo ya ukimwi katika jamii zetu.

Akifafanua zaidi alisema kuwa ikiwa mwanaume au mwanamke atakuwa na wanawake wengine nje ya ndoa yake anaweza kumsababishia mwenzie kupata maambukizo ya ugonjwa wa ukimwi.

No comments:

Post a Comment