Hivi karibuni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini imewapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano.
Mafunzo hayo yameendeshwa na Taasisi ya Thomson Foundation na kugharamiwa na Serikali ya Uingereza.
Pichani Mkufunzi wa Mafunzo David Wiggins (katikati) akifurahia zawadi ya shati la kitenge baada ya kukabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Judith Mhina (kushoto ) kwaniaba ya wenzake, (kulia) ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
Moja ya jengo zuri la kisasa liliopo katika muungano wa barabara ya mtaa wa Bibi Titi na mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam linaitwa UHURU HEIGHTS.
Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwa katika picha ya pamoja. baada ya kumaliza mafunzo ya jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kama facebook,twitter, flickr nablogs.
Mkufunzi kutoka Uiengereza David Wiggins akiwaaga Maafisa Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) baada ya kumaliza mafunzo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Ujasiramali upo wa aina nyingi ili kupata pesa za kujikimu ni lazime ujishughulishe kufanya kazi na kuweza kupata pesa. Pichani kijana wa mtaani akiosha kioo cha moja ya gari lililokuwa katika foleni eneo la barabara ya Morocco jijini Dar es Salaam kama alivyonaswa na kamera ya Mwanakombo Jumaa, leo mchana.
Ujenzi wa upanuzi wa barabara wa mwendo kasi katika ya barabara ya Morogoro ukiendelea katika eneo la Magomeni Mapipa, ujenzi huo utakapomalizika utarahisisha usafiri katika jiji la Dar es Salaam na kupunguza msongamano wa magari. Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment