Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Sunday 24 March 2013

SEBASTIAN VETTEL AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA MAGARI.....FORMULA 1 GRAND PRIX.

 
 
Kijana wa Kijerumani machachari anaewalaza macho madereva wenzie, Sebastian Vettel akiwa na kikombe chake cha Malaysia wikiendi .
..................................
 
SEBASTIAN VETTEL Kijana wa Kijerumani anaetesa katika mashindano ya Magari ya Ulimwenguni (Formula 1) amechukua Ushindi katika wikiendi ya mashindano hayo ya Malaysia. Formula 1 ikiwa katika wikiendi yake ya pili kwa msimu huu, ilikuwa Malaysia ambapo Mshindi wa Pili alikuwa Mark Webber (M-Australia), na ambae anaendesha gari ya timu moja na Sebastian Vetter , wote madereva wa RED BULL.
Lewis Hamilton , aliehamia timu ya MERCEDES  kutoka timu yake ya zamani na ambayo aliendeshea tangu aanze kuwa dereva McLAREN , alichukua nafasi ya 3.
 
Ushindi huu wa Vettel, haukupokelewa vizuri na dereva mwenzake Webber kwa kuwa Webber anaamini yeye ndie alikuwa Mshindi kama Vettel angefuata maagizo ya Timu. Redio ya timu ilisikika ikiwaambia madereva hao kuwa wazime injini (yaani wasiendelee kukimbizana) na badala yake wamalize mbio hizo katika sehemu zao. Wakati huo Webber ndio alikuwa akiongoza lakini cha kushangaza bwana mdogo Vettel hakusikiliza maagizo hayo na akaamua kukimbiza gari yake na kumpita mwenzie alipopata upenyo.  Jambo ambalo aliomba samahani baada ya Mechi kuisha !!!
 
Hamilton nae ingawa kamaliza wa tatu , alikiri kuwa labda hiyo nafasi angechukua mwenza timu wake Nico Rosberg kwa kuwa na nao walikuwa na yao kwenye Timu . Uongozi ulimwambia Rosberg asikimbie sana ili aangalie matairi wakati Rosberg alikuwa ana spidi kumpita Hamilton na bila shaka angempita kuchukua nafasi ya tatu. Lakini Rosberg hakumind kama alivyomind Webber ....
 
Sisi tunasema Pole Webber siku nyingine kuwa sharp na usiwasikilize hao mabosi zako kama mwenzio ujanja kuwahi ......
 
 
Mashine ndio  hizi .............
 
 
Washindi wakiwa kwenye "Podium" huu ndio mpango mzima wa katikati mshindi wa kwanza na hiyo inaitwa "pole position" , wa kulia mshindi wa pili  na wa tatu anakaa kushoto.
 
Race inayofuata iko China...........
 
 

No comments:

Post a Comment