Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Wednesday 10 April 2013

KUTOKA FORBES MATAJIRI WATANO WA MUZIKI WA 'HIP -HOP " MAREKANI KWA MWAKA 2013 ...........




Hip-Hop's Wealthiest Artists 2013
Sean "Diddy"Combs ........Baba Lao la Utajiri kwenye Hip Hop music .


Sean "Diddy" Combs  The Artist formely knowns as Puff Daddy 
Amechukua namba 1 kwa hiyo tumuite "Baba Lao"  akiwa na Utajiri wa jumla ya Dola za Kimarekani Millioni $580. Cha kushangaza inasemekana utajiri wake huu asilimia kubwa hajaupatia kwenye muziki bali ni mahusiano yake ya kibiashara mbali na muziki kama yale na kampuni ya Diageo's Ciroc. Mkataba wake na kampuni hii unamlipa mamilioni ya fedha kwa mwaka na pale itakapotokea itauzwa basi anatakiwa kulipwa mamia ya mamilioni

The No. 2 spot goes to Shawn “Jay-Z” Carter, with a net worth of $475 million. 
 Mume wa Beyonce a.k.a Baba Ivy Blue sijui Blue Ivy amechukua nafasi ya pili akiwa na utajiri wa jumla ya Dola za Kimarekani $475. Kati ya hizo millioni $204 zimetoka kwa mauzo ya kampuni yake ya RocaWear mwaka 2007 na nyingne milioni $150 zikiwa za mkataba wake na Live Nation mwaka 2008. Na licha ya hayo bado anaingiza pesa kwenye hisa zake na kampuni za Roc Nation, Carol's Daughter na michezoni Brooklyn Nets, na nyingine nyingi tuu ikiwemo mikataba mipya na Duracell  na makampuni ya vinywaji. Kama asemavyo mwenyewe Jigga Man "Wach the Throne ". 

Andre “Dr. Dre” Young ranks third with $350 million, 
Mkongwe wa fani hii Dr Dre nae ameibuka katika nafasi ya tatu akiwa na kiasi cha Mamilioni $350 ya dola za kimarekani. Pesa hizi asilimia kubwa ni kupitia "Beats by Dr Dre headphones'. Dr aliuza asilimia 51 ya biashara yake hiyo ya "headphones" kwa kampuni ya simu HTC mwaka 2011. Baada ya mwaka kupita 2012 Dr Dre na wenzake wakanunua nusu ya asilimia walizouza kwa HTC yaani 25.5 na mpaka sasa kampuni hiyo inazidi kukua na mauzo ya yanaongezea kwani "Headphone" za Beats sasa zimeshikilia asilimia 65 ya soko hilo.  Sisi tunasema Dr Dre ni mfalme wa Beats toka enzi so well done.

Bryan “Birdman” Williams owns the No. 4 spot, 
Ni mmiliki wa lebo ya muziki iliyowaajiri mastaa wakubwa wa sasa akina Drake, Nicki Minaj and Lil wayne yaani Birdman wa  "Cash Money, Young Money" akiwa na utajiri wa dola za marekani $150.  Habari Lil Wayne nae amevuka Dola milioni $100 hivi karibuni lakini yuko nje ya hawa watano. Bosi Birdman hivi karibuni amezindua lebo ya mavazi akiita YMCMB na kinywaji cha pombe. Haya Mwakani sijui utakuwa umepanda au ndio mfanyakazi wako Lil Wayne atakupita juu ....sii tunasubiri kuona Mungu akipenda.

Rounding out the list is Curtis “50 Cent” Jackson at $125 million.
 Wa mwisho ni Mwanafunzi mmoja wa Dr. Dre na Slim Shaddy (Duu amempita Slim Shady ) .50 Cent  mwenye kiasi cha dola za kimarekani milioni $125 anafunga dimba listi hii. Huyu nae ni mhangaikaji mkubwa maana huo utajiri wake  unatoka mbali na kwenye mauzo ya muziki wake, pia ana vitu mbalimbali kama "vide games", Vitabu  , na hususan malipo aliyoyapata kwenye hisa zake katika kampuni ya maji ya vitamin Glaceau ilipouzwa kwa Coca Cola mwaka 2007.


TWIGA VOICE TUNAWAPA HONGERA NA KUSEMA MAISHA NI KUPANDA NA KUSHUKA LA MSINGI KUJIPANGA .....LABDA MWAKANI TWIGAVOICE ITAKUWA KWENYE LIST  BAADA YA "DIDDY" KUNUNUA HISA.......

..........................................

No comments:

Post a Comment