Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Wednesday 27 March 2013

WALIYOTEKELEZA RAIS JAKAYA KIKWETE WA TANZANI NA MGENI WAKE WA KIHISTORIA RAIS XI JINPING WA CHINA

Na Neema Malley

RAIS wa china BW.XI JINPING amefungua ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julias Nyererere ulioghalimu zaidi dola bilioni 15 za kimarekani ambapo ulijengwa kwa msaada wa Serikali ya China aliutoa kama zawadi kwa ajili ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na kutoa udhamini kwa wanafunzi 18,000 kwenda kusoma nchini China maswala ya teknolojia

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akifungua ukumbi huo Rais Jinping alisema uhusiano wa Tanzania na China ni wa muda mrefu lakini mbali na hilo China itatoa udhamini wa wanafunzi hao kusoma nchini humo ambapo udhamini huo utakuwa na lengo la kukuza uhusiano uliopo kati ya  Tanzania na China uliopo muda mrefu ambapo ulianzishwa na  marais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julias  Nyerere na rais wa zamani wa China Bw.Mao

Aidha alisema kuwa mataifa makubwa hayatakiwi kuyaonea mataifa madogo ambayo yanaendelea hivyo China pamoja na kuwa na uhusiano mzuri na bara la Afrika na sehemu zingine kamwe haitaingilia maswala ya ndani ya nchi husika jambo la muhimu zaidi ni kuha kikisha kuwa  umoja na amani vinadumu ili kuleta maendeleo kwa watu afrika.

Pia alisema kuwa China itatoa dola bilioni 20 kwa mwaka 2013-15 kwa nchi za Afrika ili kuweza kuisaidia miradi ya mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara,maji na elimu lakini

Hata hivyo Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa uhusiano wa nchi hizi mbili  ulianza miaka 50 iliyopita ambapo ulijengwa na aliyekuwa balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Dkt.Salim Ahmed Salim alipigania sana nchi ya china kuwa mwanachama wa umoja wa Mataifa miaka ya 1965.

"Urafiki wa China na Tanzania ni wa muda mrefu kwani China iwemeweza kujenga reli ya Tazara,kiwanda cha urafiki ambapo licha ya hayo lakini imeendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali" alisema Kikwete.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdulahman Kinana alisema kuwa kutokana na hotuba iliyotolewa na Raisi huyo inaonekana kuwa misaada mingi imeelekezwa katika maswala ya kijamii zaidi kwa kuwekeza katika swala la elimu,maji na hata sayansi ya habari kwani hivyo ndio vitu muhimu katika nchi.

Alisema kitu alichojifunza wakati akiwa nchini China kuwa wananchi wake wanafanya kazi kwa bidii pamoja na kujitahidi kujipanga katika kusimamia kazi zao

Waziri wa Afrika Mashariki Bw,Samwel Sitta alisema kutokana na hotuba aliyoitoa kuhusu njanya za elimu China  itaweza kusaidia watu wa Afrika kwa kutoa ufadhili katika fani mbali mbali ambapo wao pia walipitia njia hiyo hadi kufikia hapo walipo.


Rais huyo wa China alikuwa na Ziara ya siku mbili nchini na alisaini mikataba 16 kati ya 17 ambapo moja kati ya mikataba hiyo ni ujenzi wa bandari ya bagamoyo ambayo itakuwa kubwa kuliko zote katika ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara ambapo itajengwa kwa gharama ya dola bilioni 10 za kimarekani.

Mikataba mingine ambayo ilisainiwa ni makataba wa utekelezaji wa mpango wa ushirikiano katika utamaduni kati ya mwaka 2013-2016 na kuanzishwa na kujengwa kwa kituo cha utamaduni cha China nchini Tanzania na makataba wa mauziano ya bidhaa zitokanazo na zao la tumbaku. 

pia alipata fursa ya kuzungumza na raia wa China wanaoishi nchini ambapo alimalizia ziara yake kwa kutembelea makaburi ya wachina yaliyopo gongolamboto na kisha kuondoka nchini.

Hiyo ni ziara yake ya pili tangu kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo ambapo aliwasili nchini akitokea nchini Urusi akiongozana na mkewe Bi.Pen Liyuan akiwa na wanahabarii 82.

No comments:

Post a Comment