Leo
kulikuwa na uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasit mjini Arusha. Mgeni rasmi alikuwa
Mwakilishi wa Papa toka Vatican. Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na
mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa kutoka mataifa
mbalimbali.
Mtoto
mmoja ameeleza kuwa aliona watu waliokuwa kwenye mini bus wakirusha kitu
kuelekea kwenye mkusanyiko wa wakristo waliokuwepo kwenye
ibada.
Taarifa
zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa. Inasadikiwa
kuwa wapo waliokufa lakini haijathibitika. Muda huu vyombo vyote vya usalama
vipo eneo la tukio.
Hivi sasa kuna taharuki kubwa, na kuna taarifa ya milipuko mingine, haijulikani kama ni ya washambuliaji au ya polisi, mbali na eneo la ibada.
Nawapeni
pole nyingi waliokumbwa na mkasa huu, wakatoliki, wakristo wote na wanaolitakia
amani Taifa letu.
Taarifa kutoka mkoani Arusha ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa kuna mlipuko mkubwa mfano wa bomu umejitokeza katika kanisa la RC Arusha na kujeruhi baadhi ya waumini.
Mlipuko huo unadaiwa kusababisha taharuki kubwa katika mji wa Arusha na kuendelea kuiweka nchi katika hali tete zaidi .
mwandishi maalum wa mtandao huu kutoka Arusha anasema kuwa tukio hilo limetokea katika parokia ya Olasit mjini Arusha na bado jitihada za uokoaji zinaendelea kufanyika.
No comments:
Post a Comment