SHEIKH PONDA ISSA PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MWAKA MMOJA
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo imemuhukumu Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu wa Jumuiya na Taasisi za ki-Islam Tanzania kifungo cha nje kwa muda wa mwaka mmoja huku washitakiwa wengine wakaiachiwa huru.
Itakumbukwa kwamba Sheikh Ponda na watuhumiwa wengine wapatao 49 walishitakiwa kwa madai kwamba, Oktoba 12 mwaka 2012, ktk maeneo ya Chang’ombe Markaz, Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa, waliingia kwa jinai, walivamia ardhi ambayo ni kiwanja mali ya Agritanza Limited kwa nia ya kujimilikisha. Wanadaiwa kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huo, walijimilikisha kiwanja hicho kwa lazima katika hali ya uvunjifu wa amani na wanadaiwa kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vikiwa na thamani ya Sh milioni 59 mali ya Agritanza Limited.
“Shtaka la tano linamkabili mshitakiwa wa kwanza, Ponda Issa Ponda, unadaiwa kati ya Oktoba 10 na 16 mwaka huu, Chang’ombe Markaz, uliwashawishi wafuasi wako kutenda makosa'.
“Shtaka la tano linamkabili mshitakiwa wa kwanza, Ponda Issa Ponda, unadaiwa kati ya Oktoba 10 na 16 mwaka huu, Chang’ombe Markaz, uliwashawishi wafuasi wako kutenda makosa'.
Akifafanua sababu za msingi za adhabu hiyo hakimu alieleza kwa mukhtassar kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya sheikh huyo pamoja na washitakiwa wengine na tukio walilodaiwa kuhusika nalo, mgogoro huo ulikuwa ni wa ardhi haukustahili kisheria kuhukumia ktk mahakama hiyo, ni uhakika usiopingika kwamba mali ya Waqfu hairuhusiwi kuuzwa kisheria ya ki-Islam kwahiyo, hakukua na uhalali wa kuuzwa kiwanja hicho na mengineyo.
Hakimu badala yake aliwashauri Waislam kufuata taratibu za kisheria za kuipata ardhi hiyo.
No comments:
Post a Comment