Watu karibu 15 wamepoteza maisha na takriban 160 kujeruhiwa vibaya ktk mlipuko mkubwa uliotokea ktk kiwanda cha mbolea cha Waco ktk mji wa Texas nchini Marekani.
Mlipuko huo, mbali watu kupoteza maisha na kujeruhiwa vibaya , vilevile umeleta hasara kubwa ya kuharibiwa mali, majumba, magari na kadhalika.
Akielezea mazingira yalivyokua mmoja wa mashahidi aliyejulikana kwa jina la Debby Marak alisema ‘ilikua ni kama kuona tornado. Vitu vilirushwa hewani na kuzagaa kila mahali. Vikundi vya zimamoto na polisi bado vinaendelea kutoa juhudi kubwa ili kupunguza madhara zaidi yasitokee.
Hili ni tukio la mlipuko pili wiki hii Nchini Marekani wakati juzi katika Mji wa Boston wakati wa mbio za Marathon za mji huo kulitokea Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni mabomu uliua wananchi 3 na kujeruhi 170. Ni masaa zaidi ya 48 na bado hakuna alieshikiliwa kwa tukio hilo.
..........................................................
No comments:
Post a Comment