kwa hisani ya fullshangweblog.com
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana kulia akizungumza na Mohamed Seif Khatib katikati na Mjumbe wa Katibu wa NEC Idara ya Oganizesheni na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris mara baada ya kuwasili Wilayani Gairo wakitokea Wilayani Kilosa ambako kabla ya kuondoka kulifanyika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kilosa Town mjini Kilosa pia ilifanyika mikutano ya ndani ambapo Katibu Mkuu aliongea na viongozi wa mashina, Madiwani wenyeviti, wajumbe na waasisi wa chama hicho ikiwani pamoja na kufungua mashina katika kuimarisha chama na kukagua baadhi ya shughuli za maendeleo, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Wapogolo kikicheza ngoma hiyo kabla ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kilosa Town na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na wafuasi wa chama hicho
Kwaya ya CCM Kilosa ikiimba katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kilosa Town
Nd.Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi chama cha Mapinduzi akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Kilosa Town uliofanyika mjini Kilosa
Kilosa leo
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Kilosa wakimsikiliza Ndugu Abdurahman Kinana wakati alipokutana nao leo katika mkutano wa ndani mjini
Kilosa
Kilosa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Datomax Selanyika Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi wakati alipokuwa akimuelezea faida za kuhifadhi Mbuga za wanyama na kutunza mazingira ya mbuga hizo, Datomax pia amezungumzia mpango wa kuihamisha barabara ya lami itokayo Dar es salaam kwenda Tunduma ambayo imekatisha katika mbuga hiyo na faida za kuihamisha
--------------------------------------
No comments:
Post a Comment