Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Thursday 18 April 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BI KIDUDE LEO.....


kwa hisani ya www.sufianimafoto.com 
 
Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu.
 
 
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.
 
 
Maelfu ya wananchi na waumini wa dini ya kiislamu waliofurika katika msikiti wa Mwembeshauri katika maziko ya Marehemu Bikidude leo, wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa marehemu huyo wakati wakielekea mazikoni kijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati Unguja.
 
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Msanii mkongwe wa Muziki wa Mwambao (Taarab) Tanzania,Marehemu Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo mchana.
 
 
 

Rais wa  jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kuli) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia waliokaa) Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif, na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiomba dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka 'Kidude' aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja.tumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo mchana.
 
-----------------------------------------
 

No comments:

Post a Comment