Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Monday 8 April 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MKEWE MAMA SALMA WAWASILI NAIROBI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS UHURU KENYATA.

















Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013



















Mheshimiwa Rais Kikwete akipokea maua kutoka kwa binti  baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi .

Mama Salma Nae akipokea maua mazuri  kwa binti mzuri baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.  Na Kwa hakika Mama yetu Salma amependeza sana na rangi hizi za nguo.



















Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wakipiga picha ya pamoja na wasichana waliowazawadia mashada ya maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani kesho April 9, 2013


















Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha wageni katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Mama Salma Kikwete na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian wamesimama pembeni  wakiangalia pamoja na wenyeji wao (picha zote na IKULU)

No comments:

Post a Comment