habari na picha kwa hisani ya Fullshangweblog
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Luaha Kilosa Mkoani Morogoro wakati yeye akiongozana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakati katibu mkuu huyo alipofanya ziara katika eneo hilo, Katibu mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi ya kuhimiza maendeleo na kukagua miradi ya maendeleo ili kuisimamia serikali katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwahamasiha wananchi katika kushiriki shughuli za maendeleo (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE -KILOSA)
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa Luaha Kilosa mkoani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na Mohamed Seif Khatib Mjumbe wa NEC Oganizesheni na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Luaha Kilosa
Ndugu Mohamed Seif Khatib akizungumza na wananchi wa Luaha
MAHENGE
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akishuka kutoka kwenye Kivuko cha Mto Kilomberomapema leo kuelekea Mahenge ambako aliongea na wananchi na kuamsha ari ya kushiriki katika shughuli za maendeleo, vilevile kukagua uhai wa CCM na shughuli za maendeleo katika kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akipata vitumbua baada ya kununua kutoka kwa mmoja wa akina mama mara baada ya kuvuka mto Kilombero na ujumbe wake
Pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye naye alipata Kitumbua .
Nape Nnauye akijaribu kupanda katika moja ya mitumbwi ya wavuvi wa mto Kilombero.
Haji Mponda kulia Mbunge wa Ulanga Magharibi akizungumza na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana mara baada ya kumpokea katika mto Kilombero .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akitembelea karakana ya mafundi Ushirika wa mafundi seremala wa Ulanga ambao wanatengeneza mizinga ya nyuki.
Ndugu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM Ulanga mara baada ya kuwasili ofisini hapo kwa ajiji ya kupata taarifa za chama
Wajumbe mbalimbali wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Katibu Mkuu Ndugu Abdurahman Kinana.
--------------------------------------------------------
No comments:
Post a Comment