Mkongwe wa Muziki wa Taarab nchini Tanzania, Fatma bint Baraka maarufu kama Bi Kidude amefariki dunia leo nchini Tanzania, Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Bi Kidude ambae haujulikani umri wake wa uhakika, lakini inasemekana kuwa alikuwa na takriban Miaka 102 alizaliwa visiwa vya Zanzibar na alijipatia umaarufu sana kwa muziki wa Taarab katiak majukwaa tofauti ya ndani na nje ya Nchi, mpaka bara la Ulaya, na ni kutokana na sanaa hii aliweza vilevile kuitangaza nchi yake ya Tanzania na hususan visiwa vya Zanzibar.
Bi Kidude anaacha Historia ya kuwa Mwanasanaa wa muziki aliyeimba na kuitumikia sanaa yake hii kwa muda mrefu na kwa uhai wake wote bila ya kustaafu kutokana na Umri .
MUNGU AIPUMZISHE PEMA ROHO YA BI KIDUDE.
No comments:
Post a Comment