Balozi mpya mteule wa Tanzania nchini Comoro, Mheshimiwa Chabaka F. Kilumanga(nne kushoto), akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa na Wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania - London, baada ya kukaribishwa kwa shangwe za kumpongeza rasmi kwa kuteuliwa kwake kuwa Balozi nchini Comoro. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Chabaka Kilumanga kuwa Balozi wa Tanzania, nchini Comoro, na Kabla ya uteuzi huo, Bwana Chabaka Kilumanga alikuwa Naibu Balozi katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza
No comments:
Post a Comment