Breaking News, Home News, international News, Comprehensive, up-to-date News coverage, aggregated from sources all over the world...

Sunday 31 March 2013

DAVID MILIBAND AACHIA NGAZI BODI YA TIMU YA SUNDERLAND BAADA YA KOCHA MPYA KUPATIKANA

Pichani ni Mh. Rais Kikwete akikabidhiwa jezi ya Timu ya Sunderland na Mwenyekiti wa Club Ellis Short hiyo na aliyesimama kwa shangwe pembeni ya Mh. Rais ndio Mbunge machachari David Millliband ambae alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Sunderland. Picha hii ilipigwa Ikulu ya Tanzania Viongaozi hao walipomtembelea  Mh.Rais mwishoni mwa mwaka 2012.
 
Mbunge Maarufu wa Chama cha kisiasa cha Labour Nchini Uingereza , David Milliband ambae alikuwa ni Makamu Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Timu ya Mpira ya Sunderland ameachia ngazi vyeo hivyo vilivyomfanya akae kwenye Bodi ya Mpira ya Timu hiyo baada ya Timu ya Sunderland kumchagua muItaliano Paolo Di Canio kama Manager /Kocha Mpya .
 
Sababu aliyoitoa kuachana na Club hiyo baada ya uteuzi huo ni kuwa ni kutokana na mtazamo wa kisiasa wa nyuma wa Kocha huyo mpya wa Sunderland Di Canio ambae miaka iliyopita amekuwa akijulikana kama ni mtu mweye msimamo mkali wa kisiasa na mbaguzi.  
 
 David Milliband ni mbunge  maarufu wa Labour, ambae mwaka 2011 alishindwa na mdogo wake Ed Milliband katika kinyang'anyiro cha kuwa Kiongozi wa Chama Hicho cha Upinzani NChini Uingereza. Hii ilitokea licha ya kuwa wengi walitegemea kuwa yeye ndie angekuwa Kiongozi mpya wa Labour kutokana na Utendaji wake.
 
 David Milliband ambae vilevile wiki iliyopita alitangaza kuwa anaachia ngazi kama Mbunge wa Labour katika kiti cha jimbo la South Shields kutokana na kupata kazi Nchi ya Marekani, ameitakia club ya Sunderland kila la kheri na kuesema kuwa ni Club inayofanya mambo mengi ya maana katika miji ya Kaskazini mwa Uingereza. Sehemu ambayo inajulikana kwa uduni wa maisha.
 
 
TWIGAVOICE  TUNAWATAKIA DAVID MILLIBAND  NA VILEVILE TIMU YA SUNDERLAND  KILA LA KHERI  
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment